Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

ULEGA: SHILLINGI BILIONI 106 KUIMARISHA MATENGENEZO YA BARABARA NCHINI.


📌Alishukuru Bunge pamoja na Kamati ya Bunge kwa michango yao.

Wizara ya Ujenzi imeishukuru Bunge kwa kupitisha sheria ya fedha za Mfuko wa Barabara na kutoa maelekezo ya fedha hizo kupelekwa moja kwa moja kwenye Mfuko wa Barabara.

Akizungumza mkoani Dodoma Bungeni leo Agosti 27, 2026 Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema Serikali sasa imetekeleza agizo hilo kwa vitendo, ambapo katika miezi ya Julai na Agosti jumla ya shilingi Bilioni 106 zimeingizwa moja kwa moja kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenda kwenye Mfuko wa Barabara.

Amesema fedha hizo zitaiwezesha Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kufanya matengenezo ya barabara mbalimbali nchini, ikiwemo barabara ya Singida - Mbuyuni- Dareda -  Babati–Arusha, kwa lengo la kuondoa mashimo na kurekebisha maeneo yaliyoharibika.

Aidha, Waziri Ulega amesema TANROADS imejipanga kutumia fedha hizo kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño, ili kuhakikisha barabara zote nchini zinaendelea kupitika wakati wote.