Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi mara baada ya kufunga Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo , mkoani Singida, Februari 12, 2025.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza na waandishi wa habari wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea mradi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato, jijini Dodoma.
Muonekano wa Jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimatafa wa Msalato, jiini Dodoma ambalo kwa sasa limefika asilimia 51.2
Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema akisalimiana na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega mara baada ya kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaofanyika jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 27 hadi 28 Januari 2025.
International Seminar on Transport Asset Management
International Seminar on Transport Asset Management
Muonekano wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jijini Dodoma ambalo ujenzi wake bado unaendelea.
Muonekano wa Daraja la Lukuledi likiendelea kujengwa Mkoani Lindi
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu (DAHRM), Bw. Mrisho Mrisho akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Mhandisi Mussa Bally Natty na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Mhandisi Rashidi Kalimbaga katika ofisi za Wizara ya Ujenzi, jijini Dodoma.
Kazi za ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga zikiendelea Mkoani Rukwa. Ujenzi wa Uwanja huo umefikia asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2025.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2025.
Muonekano wa barabara ya Mianzini-Olemringaringa-Shambasi-Ngaramtoni (KM18) ambapo ujenzi wake unaendelea jijini Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akimkabidhi Mkandarasi Mkandarasi Jiangx Geo Engineering anayetekeleza ujenzi wa daraja la Tanganyeti wilayani Longido (m 40) katika barabara ya Arusha-Namanga kwa gharama ya Shilingi bilioni 4.6, Mkoani Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiteta jambo na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akitoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Reginald Massawe wakati akikagua barabara ya Arusha-Holili ambayo iliathiriwa na mvua katika maeneo ya Kwamsomali na King'ori.
Muonekano wa juu wa eneo lililokuwepo Daraja la Gonja Mpirani ambalo limekatika na kufunga mawasiliano ya barabara Mkoani Kilimanjaro. Daraja hilo lipo katika barabara ya Same-Mkomazi (km 105) na linaunganisha Kata za Ndungu na Maore.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu wakati alipofika katika Daraja la Gonja Mpirani lililokatika na kufunga mawasiliano Mkoani humo. Daraja hilo lipo katika barabara ya Same-Mkomazi Km 105 na linaunganisha Kata za Ndungu na Maore.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando, Mkoani Tanga.
Muonekano wa barabara ya Handeni-Mafuleta (km 20) inayojengwa kwa kiwango cha lami na Mkandarasi Henan Highway Engineering Group (HEGO), mkoani Tanga.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akikagua ujenzi wa barabara ya Handeni-Mafuleta (km 20) inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Tanga.
Muonekano wa juu wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 linalojengwa mkoani Tanga.
Muonekano wa kazi za ujenzi wa barabara ya Tungamaa-Mkwaja-Mkange (km 95.2) kwa kiwango cha lami zikiendelea, Mkoani Tanga.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akitoa maelekezo kwa Mkandarasi M/s China Railway 15 Bureau Group Corporation anayejenga barabara ya Tungamaa-Mkwaja-Mkange (km 95.2) kwa kiwango cha lami, mkoani Tanga.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli wakikagua ujenzi wa barabara ya Kimara - Bonyokwa - Kinyerezi (km 7), mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akitoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi John Mkumbo kuhusu usimamizi wa ujenzi wa barabara ya Kigamboni inayoendelea kujengwa mkoani Dar es Salaam.