Habari
WIZARA YA UJENZI YANG’ARA TUZO ZA TPSIA 2025
Wizara ya Ujenzi imetunukiwa tuzo ya Wizara Iliyofanya kazi kwa kiwango bora 2025 katika Tuzo za Utumishi wa Umma na Ubunifu (TPSIA 2025), zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam usiku wa kuamkia tarehe 17, Disemba 2025.
Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi, Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali Watu Bi Lizeta Kivenule amesema Wizara ya Ujenzi inatoa shukrani kwa waandaaji wa Tuzo hizo kwa kutambua mchango unaotolewa na Wizara ya Ujenzi kwa kuhudumia watu, kazi na mambo mbalimbali pamoja na taasisi zilizopo chini yake.
"Tuzo hizi ni heshima naamini italeta ari kufanya kazi kwa bidii, kujitoa kuhudumia wanachi na hivyo kuongeza uchumi kwa taifa letu", amesema Bi Lizeta Kivenule.
Tuzo hiyo ni uthibitisho wa jitihada za Wizara katika kuboresha utoaji wa huduma, kuimarisha ubunifu na kuchangia maendeleo ya miundombinu na Uchumi wa Taifa.
