Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

MENEJIMENTI WIZARA YA UJENZI YAPATA ELIMU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA KATIKA MIRADI YA BARABARA


Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi leo, Juni 4, 2026, imepata elimu kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika miradi ya barabara ilipotembelea banda la Wizara ya Ujenzi pamoja na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Kupitia banda hilo, Menejimenti ilipata fursa ya kujifunza kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na sekta ya Ujenzi katika kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa na kulindwa wakati wa utekelezaji wa miradi.

Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na TANROADS inashiriki katika Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026 yanayolenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa maendeleo endelevu.

Kilele cha maadhimisho hayo kinatarajiwa kufanyika kesho, Juni 5, 2026, yakiongozwa na kaulimbiu isemayo: “Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.”