Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

SIMBACHAWENE AIPONGEZA TBA: UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJENGO


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene ameipongeza Wizara ya Ujenzi kupitia  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Ujenzi na usimamizi wa majengo ya Serikali ikiwemo ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma.

Pongezi hizo amezitoa leo Juni 17, 2025 wakati akizindua  maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Chinangali Park mkoani Dodoma ambayo yanaongozwa na kauli  mbiu inayosema "Himiza matumizi ya mifumo ya kidijitali ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji".

Mhe.Simbachawene amesema matumizi ya mifumo ya kidigitali yamerahisisha shughuli mbalimbali za kiserikali ikiwemo kutoa nafasi za ajira pia imeongeza  ufanisi  na uwajibikaji wa kazi kwenye utumish wa Umma.

Ametoa wito kwa watumishi wote  wa wizara na taasisi za umma kutumia  TEHAMA ili kuwezesha wananchi kupata taarifa kwa urahisi na haraka