Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

SEKTA BINAFSI NI MUHIMU KATIKA UWEKEZAJI WA BANDARI


Katibu Mkuu wa wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia Sekta ya Uchukuzi ,Gabriel Migire amesema  pamoja na kazi kubwa inayofanywa  Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (TPA)  ni muhimu kwa sekta binafsi kushirikishwa katika utoaji wa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi.

Migire ameyasema hayo leo Julai Mosi,2023 jijini Dar es Salaam kwenye kikao cha Maboresho ya Bandari kilichowakutanisha  wadau wa Bandari ikiwa  pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Wizara ya Ujezi na Uchukuzi pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania   TRA.

“ Ili Bandari ifanye kazi kwa ufanisi ni muhimu kwa Sekta Binafsi  kushirikiana na Serikali ili huduma katika Bandari zetu ziweze kuongeza ufaninisi , hivyo ni muhimu Sekta  kuendelea kujitokeza na kuojiongezea uwezo wa kuongeza ufanisi wa kazi,” amesema Migire.

Kwa upande wake Ashraf Khan Mdau wa Bandari kwa zaidi ya Miaka 45 anasema  Sekta Binafsi ni Muhimu kwa Kuongeza Ufanisi katika Bandari yoyote  kwa kuwa kazi ya Bandari sio kupakua na kushusha tu Shehena na Mizigo .

“ Kazi ya Bandari ni kushusha, kupakia na kusafirisha kupeleka kwenye Bandari Kavu  hii itasaidia sana kupunguza  msongamano katika Bandari “ alisema Khan. 

Naye Mwanasheria wa Wizara ya ujenzi na Uchukuzi  Sekta ya Uchukuzi  Mohamed Salum amesema katika  makubaliano  ya uwekezaji  wa Bandari  unazingatia wawekezaji wazawa hivyo kila Mwekezaji   awe na  uwezo  kufanya  kazi   na waziwa. 

Huku Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Sekta ya Uchukuzi Dokta Ally Possi  amesema Mikataba yote ya ushirikiano inazingatia Sheria ya Uwekezaji inayotumika Nchini Tanzania.