Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

MADARAJA YAIBUA FURSA ZA KIUCHUMI, YAIMARISHA USAFIRI SIMIYU


SERIKALI ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara na madaraja katika Mkoa wa Simiyu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha usafiri na usafirishaji, pamoja na kuwawezesha wananchi kufikia huduma muhimu za kijamii na kiuchumi kwa urahisi.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa madaraja ya Itembe, Mwakisandu na Mwakagula, ambayo yameendelea kuwa viungo muhimu vya mawasiliano kwa wananchi, huku yakichangia kurahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda kwenye masoko.

Akizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo, Mhandisi Henry Mlang’a kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, amesema Daraja la Itembe lenye urefu wa mita 150, pamoja na barabara za maingilio zenye urefu wa kilomita moja, limeimarisha mawasiliano kati ya Mkoa wa Simiyu na mikoa ya Kanda ya Kati na Kaskazini.

“Utekelezaji wa miundombinu hii umekuwa na umuhimu mkubwa, hususan wakati wa msimu wa mvua, ambapo baadhi ya maeneo yalikuwa yakikumbwa na changamoto za kupitika kutokana na kujaa kwa maji,” amesema Mhandisi Mlang’a.

Amesema uwepo wa miundombinu hiyo umeongeza ufanisi katika usafirishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda kwenye masoko, hatua inayowawezesha wananchi kupata masoko kwa urahisi na kupunguza gharama za usafirishaji.

Aidha, Mhandisi Mlang’a amesema TANROADS Mkoa wa Simiyu umejiandaa kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua za Elnino zinazotarajiwa kunyesha nchini ambapo wataalamu wamepelekwa katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kukagua maeneo hatarishi na kufanya matengenezo yanayohitajika.

Kwa upande wao, wananchi wa maeneo yanayohudumiwa na madaraja ya Itembe na Mwakisandu wameipongeza Serikali kwa kutekeleza miradi hiyo, wakisema imewasaidia kuondokana na changamoto za usafiri na usafirishaji zilizokuwepo awali.

Wamesema maboresho hayo ya miundombinu yamewawezesha kutumia kwa ufanisi zaidi fursa za kiuchumi, hususan katika kilimo na ufugaji, kutokana na kurahisishwa kwa usafirishaji wa mazao na mifugo kwenda kwenye masoko.

Utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea kuimarisha mtandao wa miundombinu ya usafiri katika Mkoa wa Simiyu, huku ukichangia kuongeza fursa za kiuchumi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa w