Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

KATIBU MKUU UJENZI ASISITIZA MSALATO AIRPORT KUKAMILIKA HARAKA


Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour amekagua utekelezaji wa mradi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato jijini Dodoma, na kusisitiza mradi huo ukamilike haraka.

Aidha, ameelekeza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) pamoja na Mhandisi Mshauri kuhakikisha kuwa wanamsimamia Mkandarasi Beijing Construction Engineering GroupCompany Ltd (BCEG) wa sehemu ya pili inyohusisha jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege pamoja na majengo mengine kuongeza kasi ya utekelezaji ili majengo hayo yakamilike kama ilivyopangwa kwenye mkataba.

Mradi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato unatazamiwa kufungua fursa za kiuchumi na kijamii na hivyo kuleta maendeleo jijini Dodoma na  Taifa kwa ujumla pindi utakapokamilika.