Naibu Waziri wa Ujenzi, Mha. Godfrey Kasekenya, akizungumza katika Semina jijini Dodoma, kuhusu mkakati wa kuongeza ushiriki wa wazawa kwenye miradi ya ujenzi nchini iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi kwa Kamamti ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo na viongozi wengine wakikagua urejeshaji wa miundombinu ya barabara ya Lindi –Dar es Salaam eneo la Somanga ambalo limeanza kupitika Mkoani Lindi.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam eneo la Somanga ambalo zoezi la urejeshaji wa miundombinu ya barabara hiyo imeimarishwa, Mkoani Lindi.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akimsikiliza Mkazi wa eneo la Mikereng’ende, Shaweji Kibwebwe wakati alipokuwa akisimamia zoezi la urejeshaji wa miundombinu ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam katika eneo hilo ambalo limekatika kutokana na mvua za El-Nino zilizonyesha zikiambatana na Kimbunga Hidaya na kusababisha wananchi kukwamaa kwa siku kadhaa Mkoani Lindi.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Matengenezo kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS), Dkt. Christina Kayoza na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani, Eng. Baraka Mwambage wakati akikagua kazi zinazoendelea za urejeshaji wa miundombinu ya barabara kuu ya Lindi – Dar es Salaam katika eneo la Somanga, tarehe 07 Mei, 2024 Mkoani Lindi.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Matengenezo kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS), Dkt. Christina Kayoza na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani, Eng. Baraka Mwambage wakati akikagua kazi zinazoendelea za urejeshaji wa miundombinu ya barabara kuu ya Lindi – Dar es Salaam katika eneo la Somanga, tarehe 07 Mei, 2024 Mkoani Lindi.
Kazi zikiendelea za urejeshaji wa mawasiliano ya barabara kuu ya Lindi – Dar es Salaam eneo la Somanga ambalo limekatika kutokana na mvua zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya, Mkoani Lindi.
Zoezi la Urejeshaji wa Miundombinu ya Barabara Kuu ya Lindi - Dar es Salaam katika eneo la Somanga Mkoani Lindi ukiendelea.
Zoezi la Urejeshaji wa Miundombinu ya Barabara Kuu ya Lindi - Dar es Salaam katika eneo la Somanga Mkoani Lindi ukiendelea.
Muonekano wa magari yakiwa katika zoezi la urejeshaji wa miundombinu ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam, eneo la Nanguruku ambalo limekatika kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha zikiambatana na Kimbunga Hidaya, Mkoani Lindi
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo, Mkurugenzi wa Matengenezo kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) Dkt. Christina Kayoza pamoja na timu ya Wataalamu wa TANROADS, wakikagua Miundombinu ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam ambayo mawasiliano yake yamekatika kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Lindi.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Lindi - Dar es Salama, eneo la Somanga ambalo limekatika kutokana na Mvua za El-nino zinazoendelea kunyesha Mkoani Lindi.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashunga akifafanua jambo kuhusu Mikakati ya Serikali ya kuongeza ushiriki wa Wazawa katika miradi ya ujenzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati akifungua semina hiyo iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 04 Mei, 2024.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga, Mhandisi Mwanaisha Ulenge wakati akitoa maoni kuhusu Mikakati ya Serikali ya kuongeza ushiriki wa Wazawa katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi katika Semina iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 04 Mei, 2024.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akiwa pamoja na Katibu Mkuu Balozi Aisha Amour, na viongozi mbalimbali wakikagua miundombinu ya barabara ya Mwaikibaki (Morocco-Africana), ambayo inatarajiwa kufanyiwa upanuzi kuwa njia nne, Mkoani Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akiwa pamoja na Katibu Mkuu Balozi Aisha Amour, na viongozi mbalimbali wakikagua miundombinu ya barabara ya Mwaikibaki (Morocco-Africana), ambayo inatarajiwa kufanyiwa upanuzi kuwa njia nne, Mkoani Dar es salaam.
Mafundi wakiendelea na kazi ya urejeshaiji wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha changarawe katika barabara ya Bunju B - Mpiji Magoe, Mkoani Dar es Salaam.
Muonekano wa eneo litakapojengwa Daraja la Mpiji Chini (mita 140) na barabara unganishi (km 2.3), Mkoani Dar es Salaam. Daraja hilo litaunganisha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akipita katika Daraja la muda la Mpiji Chini linalotumiwa na wananchi wakati alipokuwa akikagua hatua za maandalizi ya ujenzi wa Daraja la Mpiji Chini (mita 140) na barabara unganishi (km 2.3) litakalounganisha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akisisitiza jambo kwa Meneja Mradi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group (CRSG), Pan Jiangriang wakati alipokagua maandalizi ya ujenzi wa Daraja la Mpiji Chini (mita 140) na barabara unganishi (km 2.3) litakalounganisha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiwa na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile wakikagua jengo la abiria na mifumo ya malipo ya ukataji tiketi wa N-CARD katika eneo la Magogoni, katika ziara ya kukagua utoaji huduma za Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza na kusikiliza changamoto za wananchi wanaotumia usafiri wa kivuko katika eneo la Magogoni – Kigamboni, wakati akikagua utoaji wa huduma unaotolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mkoani Dar es Salaam
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kibada, Wilayani Kigamboni Mkoani Dar es Salaam akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua athari za miundombinu ya barabara na madaraja zilizotokana na mvua za El-Nino katika barabara ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji (km 41).
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akikagua barabara ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji (km 41) ambayo imeathiriwa na mvua zilizonyesha za El Nino Wilayani Kigamboni Mkoani Dar es salaam
Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Ujenzi wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyazi la Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) na Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara hiyo na Taasisi zake, jijini Dodoma.