Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

TANROADS KUKAGUA MIRADI YA NCHI NZIMA “KASEKENYA”


Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amewataka Wakala wa Barabara Nchini ( TANROADS) kuhakikisha wanakagua madaraja pamoja na Barabara za Nchi nzima ili kuhakikisha yanakuwa salama kipindi hiki cha Mvua zinazoendelea kunyesha.
Aidha , Kasekenya amekagua Daraja la Kitumba, linalounganisha kata ya Mirumba na Kitongoji cha Magodauni, kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda ambalo limeonekana kuanza kupata hitilafu.

Naibu Waziri Kasekenya anaendelea na Ziara yake Mkoani Katavi, ambapo atakagua Barabara, Madaraja, Ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege.