Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

RAIS SAMIA ADHAMIRIA KUUFUNGUA MKOA WA MTWARA


Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amemweleza Makamu wa Rais Mhe. Deogratius Ndejembi kuwa zaidi ya shilingi bilioni 234 zinatumika katika ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata- Masasi km 200.

Hatua hiyo inalenga kuufungua mkoa wa Mtwara kwa barabara za lami na kuchochea shughuli za kilimo, biashara na uchukuzi mkoani humo.

 "Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuwezesha Wizara ya Ujenzi ili tujenge barabara hii  na hivyo kuziunganisha wilaya zote za mkoa wa Mtwara kwa lami na  kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi", amesema Eng. Kasekenya.

Eng. Kasekenya amesisitiza kuwa barabara hiyo itakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Aidha, Eng. Kasekenya amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa maandalizi kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Newala- Kitangali- Mtama km 74 yanaendelea na usanifu umekamilika.

Makamu wa Rais Ndejembi anaendelea na ziara yake katika mikoa ya kusini ambapo baada ya mkoa wa Ruvuma sasa ameingia Mtwara.