Habari
MAWAZIRI BASHUNGWA NA MBARAWA WAKUTANA WA UJUMBE KUTOKA UJERUMANI.
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wamekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nchini Ujerumani ulioongizwa na Mhe. Michael Kellner, Makamu wa Waziri wa Wizara ya Uchumi na Mabadiliko ya Tabianchi wa Ujerumani.
Wawekezaji na Wafanyabiashara hao ni sehemu ya Ujumbe ulioambatana na Mheshimiwa, Dkt. Frank-Walter Steinmeier, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani aliyefanya ziara ya kikazi nchini kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi 1 Novemba 2023.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 31 Oktoba 2023 katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es salaam ambapo wamejadili maeneo mbalimbali ya Mashirikiano katika Sekta ya Ujenzi na Uchukuzi.
Pamoja na mambo mengine, Wawekezaji na Wafanyabiasha wa Ujerumani wameonesha nia ya kuendelea kushirikiana na Tanzania katika uendelezaji katika maeneo mbalimbali ili kukuza uchumi wa Taifa kupitia sekta hizo mbili.