Habari
MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA RUVUMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameitaka Wizara ya Ujenzi kuandaa mkakati kabambe utakaowezesha ujenzi wa barabara ya Kitai- Lituhi Km 84.5 mkoani Ruvuma kukamilika kwa kiwango cha lami ili kuchochea shughuli za kiuchumi mkoani humo.
Mhe. Ndejembi amesema hayo leo alipokagua ujenzi wa barabara hiyo sehemu ya Amanimakoro- Ruanda yenye urefu wa km 35.
"Hakikisheni mnakuja na mkakati wa haraka ili barabara yote ijengwe kwa muda mfupi na ubora ili kuchochea ukuaji wa uchumi", amesisitiza Makamu wa Rais Ndejembi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema Wizara itahakikisha inatekeleza maelekezo hayo kwa kumlipa Mkandarasi kwa wakati ili kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo.
Eng. Kasekenya ameseka ujenzi wa barabara hiyo umegawanywa katika awamu tatu ambazo ni Kitai- Amanimakoro km 5 ambazo tayari ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika, Amanimakoro-Ruanda Km 35 ujenzi wake unaendelea na Ruanda-Lituhi -Ndumbi km 50 ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Makamu wa Rais yuko mkoani Ruvuma katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.
