Habari
KASEKENYA- UJENZI MAENEO KOROFI BARABARA YA DAR -LINDI WAANZA
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Dar es salaam -Lindi katika maeneo korofi ili kuirudisha barabara hiyo kwenye viwango vya juu vya ubora.
Eng. Kasekenya amesema hayo leo katika mji wa Nangurukuru Wilayani Kilwa mkoani Lindi wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi.
" Takriban km 165 zinajengwa upya katika maeneo korofi kwenye barabara hii ambapo km 95 ziko Mkoa wa Lindi na Km 70 ziko Mkoa wa Pwani", amesisitiza Eng. Kasekenya.
Amesema ujenzi huo unafuatia kukamilika kwa madaraja katika barabara hiyo ya kiuchumi inayounganisha mkoa wa Dar es salam na mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Makamu wa Rais Ndejembi ameipongeza Wizara ya Ujenzi kwa uboreshaji wa barabara hiyo ambayo imekuwa ikipitisha magari mengi na makubwa kufuatia kupanuliwa kwa bandari ya Mtwara na ongezeko la shughuli za viwanda na uzalishaji mazao ya kilimo katika mikoa ya Kusini.
