Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

ULEGA AKAGUA UJENZI DARAJA LA JANGWANI


Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amekagua utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa Daraja la Jagwani lenye urefu wa mita 390 na barabara za maingilio zenye urefu wa mita 710 ambao ujenzi wake unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 97.1.

Waziri Ulega amefanya ukaguzi huo jijini Dar es Salaam akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour na kuridhishwa na hatua mbalimbali zinazoendelea ambapo mpaka sasa Mkandarasi amefikia asilimia 13.

Ulega ameeleza ujenzi wa Daraja hilo ni sehemu ya mkakati wa kudumu wa kuondoa changamoto ya mafuriko ya mara kwa mara yanayoathiri jiji hilo pamoja na kuboresha shughuli za usafiri na usafirishaji.

Ujenzi wa Daraja hilo unatekelezwa na Mkandarasi China Communications Construction Company na Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Leporogo Specialist Engineers akishirikiana na Afrisa Cosulting and Dong Myeong Engineering Consultants and Architecture kwa muda wa miezi 24.

Mradi wa ujenzi wa Daraja la Jangwani unafadhiliwa na Mkopo kutoka Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Msimbazi Basin Development  Project.