Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

UJENZI WA BARABARA YA NANGURUKURU - LIWALE - LINDI KM 231 KUANZA JUNI 2025 


Serikali imesema ujenzi wa barabara ya Nangurukuru-Liwale hadi Lindi yenye urefu wa kilometa 231 utaanza Juni mwaka huu ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji pamoja na kukuza shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi na Mikoa jirani.

Hayo yameelezwa  Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya wakati  akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Liwale aliyetaka kujua ni lini  Serikali itaanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami?. 

"Mhe.Spika usanifu wa barabara hiyo tayari umekamilika na ili kurahisisha ujenzi wake umegawanyika katika sehemu tatu ambapo sehemu ya kwanza ni Nangurukuru-Zinga (km 78.7), Zinga-Chonya (km 71.4) na Chonya-Liwale (km 75.7)", amesema Mhandisi Kasekenya.

Aidha, ujenzi wa barabara hiyo utaanzia sehemu ya tatu Chonya-Liwale (km 75.7), ambapo zabuni zimetangazwa na kazi inatarajiwa kuanza Juni, 2025.

Naibu Waziri Kasekenya amesema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo kwa ujumla.