Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

RAIS SAMIA ANATAKA KUONA MIRADI INAKAMILIKA KWA WAKATI.


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa Dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona miradi ya ujenzi ya barabara na madaraja inakamilika kwa wakati.

Ameyasema hayo Oktoba 2, 2023 wilayani Kyela, mkoani Mbeya wakati akizungumza na wakazi wa Wilaya hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza Dhamira kuu ya Serikali ni kuunganisha wilaya zote, mikoa yote pamoja na nchi jirani.

Aidha, Bashungwa amesema Serikali inakwenda kuinganisha Wilaya ya Kyela na Ileje iliyopo mkoani Songwe kwa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya

Isongole-Ipyana-Kasumulu-KatumbaSongwe yenye urefu wa kilometa 114 ambao hivi karibuni mkataba wa ujenzi huo utatiwa saini.

Bashungwa amepokea ombi la kuiboresha barabara ya Matema Hadi Ikombe yenye urefu wa kilometa 6.5 ambayo inaunganisha wilaya hiyo na ile ya Ludewa mkoani Njombe na kuiqgiza Wakala wa Barabara (TANROADS), kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

"Nimeshambiwa kuna barabara itayounganisha wilaya ya Kyela na Ludewa tumeichukua na barabara hiyo ikikamilika italeta mapinduzi makubwa kwa wilaya hizo", amesisitiza Bashungwa.