Habari
RAIS SAMIA AMWAPISHA WAZIRI ULEGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimwapisha Abdallah Hamis Ulega (Mb) kuwa Waziri wa Ujenzi katika hafla iliyofanyika Ikulu ndogo, Tunguu Zanzibar leo tarehe 10 Disemba, 2024.
Waziri Ulega anachukua nafasi ya Innocent Lugha Bashungwa (Mb) aliyeteuliwa na kuapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;
Kabla ya Uteuzi huo, Ulega alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.