Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

MIGIRE AWATAKA WAHARIRI KUONGEZA UFANISI


Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Bw. Gabriel Migire amewataka wahariri wa vyombo vya habari kuongeza ufanisi katika kufanya kazi.

Akifungua semina ya Wahariri wa vyombo vya Habari nchini ambayo  imeshirikisha Wahariri takribani 30 kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo televisheni,  redio, magazeti na blog imelenga katika kuwawezesha Wahariri kufahamu na kuelewa zaidi kuhusu shughuli, na masuala mbalimbali ya sekta ya Uchukuzi na Reli ili waweze kutekeleza majukumu ya utoaji wa  taarifa.

"Niipongeze TRC kwa hatua hii nzuri, Wahariri na waandishi wa Habari wanapaswa kuelimishwa kuhusu mambo tunayofanywa kwenye sekta ya Uchukuzi na wapeleke taarifa hizo kwa jamii kwa  usahihi na ufasaha" Amesema Ndugu Migire.

Aidha, Katibu Mkuu ameongeza kuwa  kutokana na umuhimu wa sekta ya Ujenzi na uchukuzi amewataka waandishi wa vyombo vya habari pamoja na Wahariri watumie weledi wao katika kupeleka taarifa kwa wananchi kwa haraka na  kwa kufuata utaratibu na usahihi ili kuepusha upotoshaji.

"Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imepewa asilimia 9.3 ya bajeti nzima ya serikali ya mwaka ambayo ni takribani tilioni 4 kila mwaka,hii inaonesha jinsi gani sekta hii ni nyeti ,kwa hiyo niwaambie Wahariri mko sehemu sahihi hapa ili mpate taarifa zakuwaeleza wananchi kuhusu miradi inayotekelezwa chini ya Wizara na Shirika la Reli" Amesema Ndugu Migire.

 Ameongeza kwa kusema kuwa Serikali na Viongozi wake wanahitaji vyombo vya habari katika utoaji taarifa na uhabarishaji umma ili kuleta usawa na uelewa kwa wananchi na pia kujenga uaminifu kati ya jamii na serikali.

 Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa amewaeleza Wahariri hao kuwa ujenzi wa Reli ya SGR  umetokana na juhudi za Maraisi  wa jamhuri  Muungano wa  Tanzania katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakua na kuongeza  na pia kuiunganisha Tanzania na nchi jirani  haswa za Ukanda wa Magharibi mwa nchi zenye malighafi nyingi haswa za madini kama Kongo na Burundi.