Habari
MAKANDARASI WATAKIWA KUZINGATIA TAALUMA

Makandarasi wa ndani wametakiwa kutumia wataalam wenye sifa katika kutekeleza shughuli zao, ili kuifanya miradi inayotekelezwa kuwa na viwango na kudumu kwa muda mrefu kulingana na vigezo vilivyowekwa kwenye mikataba.
Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi GODFREY KASEKENYA wakati akifungua mkutano wa tatu wa kikanda wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2023 ulioanadaliwa na Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Arusha kwa wadau wa ujenzi wa mikoa ya kanda ya kaskazini.
“Tasnia ya wahandisi inafanya kazi kwa viwango na kumbukeni kuwa mlikula viapo, hivyo ni lazima kuzingatia hilo katika utekelezaji wa majukumu yenu, maana miradi ikiwa chini ya kiwango tunawatazama nyinyi kama watu wa kwanza’ amesema Naibu Waziri Kasekenya.
Naibu Waziri Kasekenya amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika miradi inayohusisha ujenzi na kwa sasa inaendelea na mikakati yake ya kushirikisha sekta binafsi ilikuongeza kasi ya utekezaji wa miradi hiyo nchini.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandishi Joseph Nyamhanga, ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kupuguza matumizi ya force akaunti hususani katika majenzi hali ambayo imeamsha tena hari ya makandarasi wa ndani kufanya kazi.
Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Makanadarisi, Mhandisi Rhoben Nkori ametoa wito kwa Makandarasi wa ndani kufanya tafiti halisi za bei za miradi ili kuwawezesha kutekeleza miraid hiyo kwani takwimu zinaonyesha kuchelewa kwa kukamilika kwa miradi kunaokana na wakandarasi hao kuweka bei ya chini.
“Tumebaini baadhi ya makandarasi huandika gharama ndogo ya ili kupata miradi lakini matokeo yake miradi inawashinda kukumilisha kwa wakati na hivyo kupoteza uaminifu kwa watoaji wa miradi ambao ni Serikali kero”.amesema Mhandisi Nkori.
Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha makandarasi kutoka mikoa sita ya kaskaskazini na mikoa jirani, ikiwemo mkoa wa Arusha,Kilimanjaro,Manyara,Tanga,Singida na Dodoma,ambapo makandarasi watajadili na kuweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta ya makandarasi nchini.