Habari
KUSUASUA KWA MRADI KASEKENYA ATOA MAELEKEZO

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya ameeleza kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa Barabara ya Malagarasi _Ilunde_Uvinza (51.1km)inayojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Kigoma.
Kasekenya , Ameyasema hayo wakati alipokagua mradi huo unaojengwa na Mkandarasi STECOL COOPERATION ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 45 mpaka sasa na unatakiwa kukamilika Januari 2024.
“Barabara hii ni muhimu inaunganisha nchi za jirani kama Congo,Rwanda na Burundi vile vile wananchi wanahitaji barabara hii kwa ajili ya shughuli zao za kiuchumi na biashara hivyo kutokukamilika kwake kwa wakati kunachelewesha maendeleo ya wananchi" amesema Kasekenya
Aidha, ameongeza kwa kumtaka Mhandisi Mshauri kuhakikisha Mkandarasi anaongeza nguvu kazi kwenye mradi pamoja na kuongeza vifaa,wafanyakazi na masaa ya kazi ya ziada Vilevile, Mkandarasi ajue sababu zinazokwamisha mradi ili zitatuliwe na mradi kumalizika kwa wakati.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma, amemhakikishia Naibu Waziri Kasekenya kusimamia mradi kwa ukaribu na kuhakikisha unamalizika kwa wakati uliopangwa.