Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

KAMATI YASISITIZA MADENI YA MAKANDARASI KULIPWA.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiagiza Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), kuhakikisha inaendelea kulipa madeni ya wakandarasi ili kuwezesha na kurahisisha utekelezaji wa miradi mingi ya ujenzi nchini kukamilika kwa haraka na kwa wakati.

Agizo hilo limetolewa leo Tarehe 16 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Selemani Kakoso, mara baada ya kupokea Taarifa ya Wizara hiyo kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha Mwezi Julai- Desemba, 2023.

“Hakikisheni Wizara mnatumia fursa mlionayo kati yenu na Wizara ya Fedha  kupunguza au kumaliza kabisa  mlolongo wa madeni kwa makandarasi wa ndani na wa nje, naamini mkilipa madeni kwa wakati na miradi itakamilika haraka”, amesema Kakoso.

Aidha, Kakoso ameipongeza Wizara kwa jitihada wanazozichukua katika suala zima la kuwajengea uwezo makandarasi wa ndani ikiwemo kutenga miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwajengea uwezo makandarasi hao ili kuweza kukuza kipato chao na Uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Kakoso amesisitiza Wizara hiyo kuisimamia TANROADS kuhakikisha inapitia kwa undani suala la mikataba ya miradi na kuangalia vipengele vyote vyenye changamoto katika mikataba hiyo ili kuokoa gharama ambazo Serikali inazipata kutokana na udhaifu wa mikataba hiyo.

Vilevile,Kakoso ameupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kwa kuendelea na zoezi lao la ufuatiliaji na ukusanyaji wa madeni kwa wapangaji wao na kusisitiza zoezi hilo kuelekezwa pia kwa Taasisi za Umma ambazo zinadaiwa na Wakala huo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi, Godfrey Kasekenya, amesema kuwa hadi kufikia Desemba, 2023 jumla ya kilometa 134.75 za Barabara kuu sawa na asilimia 97 ya mpango wa nusu mwaka zimejengwa kwa kiwango cha lami.

Kasekenya ameongeza kuwa kwa kipindi hicho utekelezaji wa madaraja mbalimbali uliendelea ikiwemo ujenzi wa daraja la Mbambe, Mbangala, Sukuma, Mpiji Chini, Mirumba, Kibakwe na Kerema Maziwa.

Kasekenya pia ametaja miradi ya Viwanja vya ndege iliyotekelezwa katika