Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA UJENZI WA ‘MSALATO AIRPORT’ NA BARABARA YA MZUNGUKO DODOMA.


Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeipongeza Serikali ya awamu sita kupitia Wizara ya Ujenzi kwa muendelezo mzuri na kasi ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato na Barabara ya Mzunguko wa Nje Dodoma (Outer Ring Road).

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati  ya  Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya mradi huo.

"Kamati inapongeza Serikali kwa miradi hii muhimu hakikisheni inakamilika kwa wakati na ubora", amesema KakosoKakoso amesema  kiwanja hicho cha ndege  cha kimataifa kina  umuhimu  mkubwa kwani kitahamasisha kilimo, biashara na huduma na hivyo kukuza uchumi.

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amemhakikishia Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge kusimamia ujenzi huo ili kuweza kukamilika kwa wakati

"Tumeongeza muda kwa Mkandarasi wa mradi hivyo kazi zinafanyika usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliokusudiwa ", amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), amesema ujenzi wa mradi umefikia asilimia 90 na unatarajiwa kukamilika  Julai mwaka huu.