Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

BASHUNGWA AJIBU HOJA ZA BARABARA MKOANI MTWARA


Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent L. Bashungwa (Mb) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanguruwe, mkoani Mtwara wakati akijibu hoja zilizoulizwa  kuhusu Sekta ya Ujenzi, tarehe 16 Septemba, 2023. 

Waziri Bashungwa, amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za miradi ya barabara ambapo wananchi wa Nanguruwe, mkoani Mtwara wamekuwa ni wanufaika wakubwa kwa ukamilikaji wa kilometa 50 za barabara kwa kiwango cha lami. 

"Ni maelekezo yako Mhe. Rais umetuelekeza Wizara ya Ujenzi pale ambapo kilometa 50 zimeishia, kazi ziendelee  katika kukamilisha kilometa nyingine 160 zilizobakia kutoka Mnivata hadi Masasi na fedha zimekwishatengwa kwa ajili ya kukamiliasha kilometa hizi,  kutakuwa na wakandarasi wawili ambao watashirikiana kwa msukumo mkubwa ili wakamilishe kwa haraka", amesema Waziri Bashungwa. 

Aidha, Ameeleza  kutambua umuhimu wa Sekta ya Gesi Nchini kuwa na fursa ya kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa wa Mtwara, Lindi na mikoa jirani pamoja na nchi jirani, Mhe. Rais ameelelekeza Wizara ya Ujenzi kufanya usanifu na upembuzi yakinifu wa barabara ya kuanzia Mtwara kuelekea Msimbasi kwenye visima vya gesi yenye urefu wa takribani kilometa 92, usanifu umekamilika na kwa mwaka huu wa fedha 2023/24 Wizara imetenga Bilioni moja kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.