Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

BALOZI AISHA AKAGUA UTAYARI WA TANROADS KUKABILIANA NA MVUA ZA EL-NINO MKOANI LINDI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour, akikagua miundombinu ya barabara na madaraja pamoja na kutoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Lindi, Mhandisi Ezra Magogo Daniel, wakati wa ziara yake mkoani humo ya kukagua utayari wa kukabiliana na athari za mvua za El-Niño zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu ameambatana na watendaji mbalimbali wa Wizara ya Ujenzi na TANROADS, akiwemo Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Ephatar Mlavi, Mkurugenzi wa Matengenezo wa TANROADS, Mhandisi Lazaro Loshilari na Mkurugenzi wa Miradi wa Wakala huo, Mhandisi Juma Kijavara.