Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

AQRB KUPEWA UFADHILI WA MAFUNZO


Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema Wizara itaendelea kutoa ufadhili wa mafunzo kwa vitendo kwa wataalamu wa Taaluma za wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi nchini.

Akizungumza Jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa,  amesema kuwa, Bodi itaanzisha mfuko wa maendeleo ya wanafunzi ili kuweza  kutenga fedha za kusaidia vijana wenye taalamu za ubunifu majengo na wakadiriaji majenzi.

“Nimeambiwa katika mwaka huu wa fedha 2023/24 Wizara ya Ujenzi imetenga kiasi cha shilingi milioni 748 kwenye bajeti yake kwa ajili ya mpango wa mafunzo wa EAPP, nia ni kuongeza idadi ya wahitimu wanaopata mafunzo hayo”, amesema Mhandisi Kasekenya

Aidha, amezielekeza Bodi za AQRB, ERB, CRB na NCC ziweze kufanya kazi kwa ukaribu na kushirikiana ili kuhakikisha kuwa Taifa linafaidika na huduma za kitaalamu zinazotolewa na wataalamu na makampuni yaliyosajiliwa na Bodi hizo.

Kwa upande wake, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi, Arch. Edwin Nnunduma amesema kuwa wanampango wa kusajili wataalamu 5000 kufikia mwaka 2026, katika kada za kati.

“Serikali kupitia Bodi hii tumejipanga kukagua miradi zaidi ya 3014 kwa Taasisi binafsi na Serikali kwa ujumla, pia ameongeza kuwa juhudi zinaendelea kuweza kusajili wataalam pamoja na Makampuni.” amesema Arch. Nnunduma

Halikadhalika, Arch. Nnnunduma amesema kuwa ili kuboresha utendaji na ufanisi wa wafanyakazi, Bodi inatarajia kuanzisha mfumo wa kieletroniki kwa watumishi wote.

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) inaendelea na Mkutano wake wa 4 kwa siku mbili jijini Dodoma.