Dira na Dhima
- Dira
Kuwa na miundombinu bora na endelevu itakayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
- Dhima
Kusimamia ubora, uhakika na usalama wa kazi za ujenzi wa barabara, madaraja, vivuko, majengo, mitambo, umeme na vifaa vya kielektroniki kwa kushirikiana na wadau kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii yanayokidhi mahitaji ya wananchi.
- Majukumu
i. Kusimamia Utekelezaji wa Sera ya Ujenzi;
ii. Kusimamia Ujenzi na Ukarabati wa Barabara na Madaraja;
iii. Kusimamia Ujenzi na Usimamizi wa Vivuko;
iv. Kusimamia Shughuli za Ufundi na Umeme;
v. Kusimamia Ujenzi na Usimamizi wa Majengo ya Serikali;
vi. Kusimamia Makandarasi na fani za Wahandisi, Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi;
vii. Kuandaa muundo wa madereva wa Serikali;
viii. Kusimamia Maendeleo ya Watumishi katika Wizara; na
ix. Kusimamia Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi (TANROADS, TEMESA, TBA, ICoT, NCC, Vikosi vya Ujenzi, RFB, AQRB, CRB na ERB).