Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Historia

Wizara ya Ujenzi ilianzishwa kwa tangazo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Gazeti la Serikali Na. 619A la tarehe 30 Agosti, 2023. Wizara ya Ujenzi ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa sera, miongozo ya ujenzi pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, majengo ya Serikali na matengenezo ya mitambo, magari na uendeshaji wa vivuko nchini.