Muonekano wa Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimati watu, Karim Mkorehe akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu katika mahafali ya tatu ya Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) yaliyofanyika tarehe 25 Novemba, 2025 mkoani Morogoro.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi, Zuhura Amani akitoa maelezo ya mradi wa barabara ya Gairo- Dodoma - Kintinku kwa Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega alipotembelea mradi huo, Novemba 22, 2025 mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 18 Novemba 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 18 Novemba 2025.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akipokea ua kutoka kwa mtumishi wa Wizara hiyo Bi. Mary Sudi , ishara ya kukaribishwa tena Wizarani hapo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akipokea ua kutoka kwa mtumishi wa Wizara hiyo Bi. Bertha Shingu, ishara ya kukaribishwa tena Wizarani hapo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Karim Mkorehe akiwa na Watumishi wa Wizara ya Ujenzi, mara baada ya kufunga mafunzo jumuishi katika kuboresha Utendaji kazi wa watumishi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Afya (CEDHA), jijini Arusha.
Watumishi wa Wizara ya Ujenzi, wakiwa katika mafunzo jumuishi katika kuboresha Utendaji kazi wa watumishi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Afya (CEDHA), jijini Arusha.
Muonekano wa Jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiangalia tuzo aliyopewa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), katika maadhimisho ya 22 ya Siku ya Wahandisi Tanzania, yaliyofanyika Septemba 26, 2025 jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Wizara ya Ujenzi na waalikwa mbalimbali wakiwa katika maadhimisho ya 22 ya Siku ya Wahandisi Tanzania yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 25, 2025
Wahandisi wakila kiapo cha utiifu katika maadhimisho ya 22 ya Siku ya Wahandisi Tanzania yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 25, 2025
Maboresho ya Mfumo wa Usimamizi wa Kazi za Matengenezo (MUM)
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi, Aisha Amour (waliokaa katikati) akiwa na wajumbe wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Wafanyakazi la Bodi ya Usajili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi Aisha Amour, akiwa na wajumbe wa Menejimenti na Mameneja wa TANROADS wa mikoa, mara baada ya kufungua mafunzo ya Uongozi kwa viongozi hao, mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la J.P Magufuli (Km 3) mkoani Mwanza Juni 19, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea banda la Wizara ya Ujenzi katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma leo Juni 19, 2025 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Ujenzi Juni 18, 2025 katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025, Chinangali Park jijini Dodoma.
Watumishi wa Wizara ya Ujenzi wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara hiyo katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma. Maonesho hayo yanaongozwa na kaulimbiu "Himiza matumizi ya mifumo ya kidijitali ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji".
Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Wakala ya Barabara (TANROADS) na wapandaji miti kutoka Jeshi la Kujenga Taifa -Makutupora wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha zoezi la upandaji miti 150 pembezoni mwa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2025.
Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Wakala ya Barabara (TANROADS) na wapandaji miti kutoka Jeshi la Kujenga Taifa -Makutupora wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha zoezi la upandaji miti 150 pembezoni mwa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2025.
Mhandisi Mkuu, Chacha Harun kutoka Kitengo cha Usalama na Mazingira, Wizara ya Ujenzi akitoa elimu kwa sehemu ya Menejimenti ya Wizara hiyo ilipotembelea na kukagua banda la Wizara ya Ujenzi na Wakala ya barabara (TANROADS), leo Juni 3, 2025 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma yanapofanyika maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2025.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi, Godfrey Kasekenya akimpa zawadi Makamu wa Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Usafirishaji wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Hyun Hwan Jin mara baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma leo, Mei 27, 2025
Muonekano wa sehemu ya barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) ambayo kwa sasa utekelezaji wake umefika zaidi ya asilimia 85.
