Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Habari

DKT. MSONDE AFUNGUA MAFUNZO YA UANDISHI WA TAARIFA KWA WATUMISHI WA WIZARA


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde amefungua mafunzo ya uandishi wa Taarifa (Report Writing) kwa Watumishi wa Wizara ya Ujenzi ambayo yameanza leo, Februari 25, 2026 katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere, wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Dkt. Msonde amesema kuwa anaamini mafunzo hayo yatasaidia kuongeza uelewa zaidi na umahiri kwa watumishi hao kuhusu taarifa mbalimbali zinazoandaliwa Wizarani hapo.

Aidha, amewataka watumishi hao kutumia mafunzo hayo kama sehemu ya kuleta mabadiliko katika Wizara hiyo hususan katika eneo la uandishi wa taarifa linalozingatia utaalamu.

Mafunzo hayo ya Siku tatu yameshirikisha Maafisa mbalimbali wa Idara na Vitengo kutoka Wizarani hapo ikiwa ni awamu ya kwanza ya mafunzo hayo.