MMQ
Temesa ina Vivuko vingapi?

TEMESA ina jumla ya vivuko 28 vinavyofanya kazi katika maeneo 20 tofauti hapa nchini. Vivuko, 26 vinafanya kazi vizuri na kivuko MV Mwanza na MV Kiu (boti ya uokoaji) vimesimama kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Orodha ya vivuko vinavosimamiwa na Temesa?

Na.

MKOA

IDADI YA VIVUKO

JINA LA KIVUKO

1.

Dar es Salaam

3

MV. Kigamboni; MV. Magogoni                           MV. Dar es Salaam

2.

Mwanza

 11

 

MV. Ukara; MV. Kome II; MV. Misungwi; MV. Sabasaba; MV. Sengerema; MV. Ujenzi; MV. Nyerere; MV. Mwanza; MV.TEMESA; na MV. KIU

3

Tanga

1

MV Pangani II

4

Morogoro

2

MV. Kilombero I; MV.Kilombero II

5

Kigoma

2

MV.Malagarasi; MV. Ilagala

6

Kagera

2

MV. Ruvuvu; MV. Kyanyabasa

7

Ruvuma

1

MV. Ruhuhu

8

Mara

2

MV. Musoma; MV. Mara

9

Pwani

1

MV. Utete

10

Geita

1

MV. Chato; MV. Tegemeo                                

11

Mtwara

2

MV. Mafanikio; MV. Kilambo

Ukarabati wa Vivuko ukoje?

Katika mwaka wa Fedha 2015/16 TEMESA watakarabati vivuko vya MV. Magogoni (DSM), MV. Pangani II (Tanga), MV. KIU (Mwanza), MV. Mwanza (Mwanza) na MV. Nyerere (Mwanza).

Ni mikakati gani TEMESA iliyojiwekea kwa mwaka huu wa Fedha 2015/16?

  1. Kutoa elimu kwa watu wanaofanya shughuli za uchafuzi wa mazingira kwenye maeneo yenye vivuko kwa njia ya vipeperushi na kushirikisha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).
  2. TEMESA inatoa ruzuku kutokana na mapato yake kwenye vivuko vyake ambavyo havijiendeshi ili kuhudumia jamii wakati wote. Vivuko ambavyo vinajiendesha vyenyewe kutokana na mapato yake pia hutumika kutoa ruzuku kwa vile visivyoweza kujiendesa ni vivuko vya Magogoni-Kigamboni (DSM), Kilombero (Morogoro), Ilagala-Kajeje (Kigoma) na Kigongo-Busisi (Mwanza). Aidha Vivuko vingine hutegemea ruzuku ya Serikali.
  3. Kuboresha huduma za vivuko na kuongeza idadi ya vivuko katika maeneo yenye uhitaji kama Magogoni na Pangani.
  4. TEMESA imejipanga vya kutosha kuhakikisha elimu ya kutosha kwa watumiaji wa vivuko inatolewa ili kuhakikisha usafiri wa vivuko unakuwa wa uhakika.